Kampuni ya Ishirini na Nne Kumi Clobal (2410) kutoka Uturuki inatarajia kuanzisha mradi wa ujenzi wa nyumba za maakazi ili jamii iweze kuishi katika mazingira bora.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa mradi huo Tolga Tugtekin amesema Nyumba hizo za kisasa zitakuwa katika maeneo ya Fumba ambapo Kampuni hiyo inafungua milango kwa Wananchi kuweza kununua Nyumba hizo mradi utakapokamilika.
Amesema kutokana na maono ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Hussein Ali Mwinyi ya kuwaletea maendeleo Wananchi wake ikiwa ni pamoja na makaazi bora ambapo Kampuni hiyo imehamasika na kuleta uwekezaji wa aina hiyo.
Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Mh.Omar Said Shaaban amesema Serikali baada ya kusaini sheria mpya ya uwekezaji imezidi kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza katika miradi mbali mbali ya maendeleo.