WAFANYA BIASHARA WAASWA KUTOFICHA SUKARI

SUKARI ZANZIBAR

Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Ushindani halali wa Biashara Mohammed Sijamini Muhammed amesema kufuatia Ukaguzi walioufanya  leo  na Tume hiyo imebaini kuwa  wapo baadhi ya Wafanya Biashara wamekuwa wakificha Bidhaa ya Sukari na wengine kuuza  kinyume na Bei elekezi iliyotangazwa na Serikali.

Akizungumza katika ukaguzi maalum wa kuangalia  Bidhaa ya Sukari kwa Wafanya Biashara  wa Soko la Mwanakwerekwe  Mkurugenzi huyo amesema  Licha ya bidhaa hiyo kuwepo kwa wingi  Sokoni lakini imeonekana kuwa wapo  baadhi ya Wafanya Biashara wanakwenda kinyume na agizo

Amesema Serikali imeamua  kupunguza ushuru   kwa baadhi ya Vyakula ikiwemo Sukari kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha  Wananchi  hasa katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya Wafanya Biashara  wa Maduka ya Mwanakwerekwe wamesema  wataendelea kutii agizo la Serikali  la kufuata Bei elekezi na kuiomba Mamlaka husika kufuatilia kwa Wauzaji  wakubwa hasa katika Ghala  

Ukaguzi huo  umeanza katika Maduka ya wafanya Biashara Soko la Mwanakwerekwe

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.