Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali wa Biashara Mohammed Sijamini Muhammed amesema kufuatia Ukaguzi walioufanya leo na Tume hiyo imebaini kuwa wapo baadhi ya Wafanya Biashara wamekuwa wakificha Bidhaa ya Sukari na wengine kuuza kinyume na Bei elekezi iliyotangazwa na Serikali.
Akizungumza katika ukaguzi maalum wa kuangalia Bidhaa ya Sukari kwa Wafanya Biashara wa Soko la Mwanakwerekwe Mkurugenzi huyo amesema Licha ya bidhaa hiyo kuwepo kwa wingi Sokoni lakini imeonekana kuwa wapo baadhi ya Wafanya Biashara wanakwenda kinyume na agizo
Amesema Serikali imeamua kupunguza ushuru kwa baadhi ya Vyakula ikiwemo Sukari kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha Wananchi hasa katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya Wafanya Biashara wa Maduka ya Mwanakwerekwe wamesema wataendelea kutii agizo la Serikali la kufuata Bei elekezi na kuiomba Mamlaka husika kufuatilia kwa Wauzaji wakubwa hasa katika Ghala
Ukaguzi huo umeanza katika Maduka ya wafanya Biashara Soko la Mwanakwerekwe