Jamhuri ya Shirikishso la Ujerman imesaini makubaliano na Tanzania ya kuipatia zaidi ya Shilingi Bilioni 193 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo katika Sekta ya Afya.
Makubaliano hayo yamesainiwa Jijini Dar Es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Tanzania Elijah Mwandumbya na Mwakilishi wa Serikali ya Shirikisho la Ujerman Marcus Von Essen
Akizungumza mara baada ya kusaini kwa makubaliano hayo Naibu Katibu Mkuu Mwandumbya amesema Serikali Tanzania itafuatilia matumizi ya Fedha hizo ili ziweze Kutumiaka katika Miradi iliyokusudiwa.
Kwa upande wake Balozi wa Ujerman Nchini Balozi Thoms Terstegen amesema Ujerman itaendelea kushirikiana na Tanzania kati nyanja mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi wa Mataifa haya.
stories
standard