Uwanzishwaji wa Wakala wa Nishati Vijijini 'REA' umeleta Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Nishati ya Umeme Vijijini baaada ya zaidi ya Vijiji 11,800 sawa na Asilimia 96 ya Vijiji vyote kufikiwa na Umeme na Asilimia Nne inatarajiwa kufikiwa na Umeme kabla ya Mwezi wa Sita Mwaka huu .
Akipokea Kamatiya kudumu ya Bunge Nishati na Maadini iliotembelea Jimbo la Chalinze Mkoa wa Pwani kuona utekelezaji wa Miradi ya 'REA' Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini 'REA' Mhandisi Hasan Saidy amesema ilipoanzishwa 'REA' Mwaka 2007 Asilimia Mbili tu ndio Umeme ulikua umefika Vijijini na sasa wameweza kufikisha Asilimia 96%.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini Mhe.David Mathayo ameitaka Serikali kutoa Elimu kwa Wananchi umuhimu wa kuunganisha Umeme na unafuu wa gharama
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Judith Kapinga amesema Mpango wa Serikali una lengo la kufikisha Umeme kwa Vitongoji vyote kama ilivofanikiwa kwa Vijiji.
Mkoa wa Pwani 'REA' imefanikiwa kufikisha Umeme kwenye Vijiji vyote 110 na zaidi ya Bilioni 44 zimetumika kukamilisha Mradi huo.