ZAIDI YA 900 MISUNGWI WAMEPATIWA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

HUDUMA ZA MATIBABU YA AFYA YA MENO

Zaidi ya   Wakazi 900 wa Kata ya Usagara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za Matibabu ya Afya ya Kinywa na Meno zilizotolewa na wadau wa Afya katika Kituo cha Afya Usagara. 

Huduma hizo zimetolewa bure kwa wakazi wa Vijiji Vitano vya Kata ya Usagara na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Tanzania Health Environment And Development Initiative Thedi na Hope Dental Centre wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno.

Wananchi waliofika kupata huduma ya uchunguzi na Matibabu wamewaomba Wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno na Wadau wengine wa Afya kuendelea kutoa Elimu hiyo kwa Jamii.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Usagara Kashinje Machibya amestushwa kusikia kuwa Tabibu wa Afya ya Kinywa na Meno wa Kituo cha Afya Usagara Jacob Ntogwisangu hajafika Kazini kwa Siku 20 bila Taarifa yoyote na ameagiza hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe dhidi yake.

Mganga wa Afya ya Kinywa na Meno Wilaya ya Misungwi, Dk. John Ng’orobi amesema zaidi ya Asilimia 80 ya Wananchi Wilayani humo wana tatizo la afya ya kinywa.

Dk. John ng’orobi – Mganga wa Afya ya Kinywa na Meno Wilaya ya Misungwi

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.