Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema katika kipindi cha Miaka Mitatu cha Uongozo wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Diplomasi ya Tanzania na Nje ya Nchi imeongezea ukilinganishwa na Miaka mingine.
Waziri Makamba ametoa kauli hiyo wakati akizindua Kamati ya kupitia majukumu na maboresho ya Kituo cha uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kilichopo Jijini Dar es salaam ambapo amesema hali hiyo imepelekea kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Nje ya Nchini
Akizungumzia Kamati hiyo Waziri Makamba amesema Kamati hiyo itatekelezwa ndani ya Miezi Mitatu ikiwa na jukumu la kuishauri
Serikali kuhusiana na uendeshwaji wa Kituo cha uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Khamis Kagasheki amesema Tanzania ilijiondoa katika Diplomasia ya Kimataifa kwa Miaka mingi hivyo kujihusisha tena katika Diplomasia hiyo kunaipa Nchi umuhimu na msimamo wa Kimaadili.
Kamati ya kupitia maboresho ya Kituo cha uhusiano wa Kimataifa cha Dkt Salim Ahmed Salim imeundwa na Wajumbe nane, ikiongozwa na Balozi Khamis Kagasheki.