UBORA WA QUR-AN NI MUHIMU DUNIANI NA KESHO AKHERA.

MASHINDANO YA QUR-AN

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Hussein Ali Mwinyi amesema ubora wa Quran ni muhimu katika maisha ya Duniani na kesho Akhera.

    Akizungumza katika Fainali ya Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Quran Tajweed Alhajj Mwinyi amesisitiza umuhimu wa Wazazi kuwahamasisha Watoto wao na Vijana ili kutekeleza Mafundisho ya Kitabu Tukufu cha Quran kwa kuisoma na kuhifadhi.

    Amewataka Walimu wanaofundisha Quran kwa njia ya Tajweed kuifikisha na kuisambaza Wilaya za Tanzania bara na Zanzibar. 

    Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo ni Ilyaas Lamhayaoui wa Morocco aliyepata Dola za Kimarekani 5000, wa Pili kutoka Misri amepata  Dola za Kimarekani 2500 na wa Tatu kutoka Iran amepata Dola za Kimarekani 1500

    Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Khidmatulquran Islamic kwa kushirikisha Nchi mbalimbali zikiwemo Msumbiji, Indonesia, Uturuki, Pakistan, Bangladesh, Misri, Comoro, Morocco, Afrika Kusini, Iran na Tanzania Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam Tarehe 23 Machi 2024.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.