Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoani Ruvuma imebaini Jumla ya Madaraja 19 ambayo yamesombwa na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani hapo katika Ripoti iliyosomwa kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo mtela Mwampamba.
Kwa upande wake Mhandisi Silvanus Ngonyani Kaimu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanazania (TARURA) amewahakikishia Wananchi kwamba TARURA ipo kazini hivyo sio tu wameishia Daraja la Mto Njoka bali wanaendelea kurekebisha mitandao yote ya Barabara ambazo ni korofi huku akihusisha na Daraja ambalo linafanyiwa usanifu ili waanze kulirekebisha
Hata hivyo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndg.Mtela Mwampamba amesema licha ya Mkoa kuwa katika nafasi nzuri ya uzalishaji wa mahindi hivyo amewataka Wananchi kutozichukia Mvua kwani mvua ni baraka hivyo waendelee na uzalishaji wa mazao yao bali kuhusu suala la Madaraja Serikali sikivu ya awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan itahakikisha inayatengeneza
Naye Ndg. Noel Nombo ameipongeza TARURA kwa ujenzi wa Daraja hilo ambalo hapo hawali walipata changamoto ya Watoto kuto kwenda Shule kwa wakati klutokana na ukosefu wa Madaraja
Vilevile Ndg.Monica Hinju yeye amempongeza na kumshukuru kwa dhati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kwakusimamia vyema utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa Daraja hilo la Njoka