Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imewataka Wahitimu Waliofaulu Kidatu cha Sita kutumia vyema fursa walizozipata za kuendelea na Masomo ya Elimu ya juu ili kutimiza malengo yao na ya Serikali ya kuzalisha Wataalamu mahiri.
Akizungumza katika Sherehe ya kuwapongeza Wanafunzi waliohitimu Kidatu cha Sita Skuli ya Lumumba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Mohammed Mussa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya juhudi kubwa za kuhakikisha sekta ya Elimu inaendelea hivyo ni vyema kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao waliokusudia.
Muakilishi wa Jimbo la Malindi Mohammed Ahmada Salum amewapongeza Walimu kwa kazi wanayoifanya ya kuwapata Wanafunzi Elimu bora
Amesema hatua hiyo itawezesha kupatikana Wataalamu wenye sifa na kukuza uchumi wa Nchi
Nao Mkuu wa Skuli hiyo Mussa Hassan Musa na Mwanafunzi wa Skuli hiyo Tunu Kasimu Paulo ni Mwanafunzi Skuli ya Lumumba na Mwalimu wamesema kwa asilimia kubwa ufaulu wa Wanafunzi umeongezeka jambo ambalo linawapa matumaini makubwa ya kuongeza za juhudi ya kusoma kwa bidiii