Wazazi wamesisitizwa kuwasimamia Watoto wao kupata msingi mzuri wa Elimu ya Dini ili waweze kuwa na maadili mema na Viongozi waadilifu wa baadae.
Akizungumza katika Mashindano Makuu ya Kuhifadhi Qur an Zoni ya Fuoni Meli Sita Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni Yussuf Hassan Iddi amesema watoto ni hazina ambayo inahitaji kusimamiwa kujifunza mambo ya Kheri yatayowasaidia kukiendeleza Kizazi hicho
Aidha amesema hivi sasa suala la uaminifu limepungua katika Jamii hivyo ni muhimu Watoto wakuzwe katika miongozo ya kuwajenga kuwa Waaminifu
Amir wa Kanda ya Fuoni Haji Sheha Ngwali amesema Qur an ndio Dira ya Maisha ya Waislam hivyo ni jukumu la Wazazi, Walezi na Walimu kuhakikisha wanaufuata muongozo wa Qur an kwa vitendo ili Watoto waweze kujifunza kutoka kwao Akhlak njema
Mashindano hayo yamewashirikisha Watoto Wakike na Kiume wenye umri wa Miaka 6 hadi 14 ambapo Washindi wa kwanza hadi wa 3 waliohifadhi Juzuu ya 1 hadi 30 walipewa zawadi na Fedha taslim akiwemo Mwanafunzi Zuhura Athmani Ali mwenye miaka 14