DKT. NCHINIMBI AELEZEA MCHANGO WA WAZEE KATIKA MAENDELEO

KATIBU MKUU CCM

    Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema maendeleo yaliyofikiwa Nchini yametokana na juhudi kubwa za kiutendaji zilizoasisiwa na Wazee wa Chama hicho waliohudumu kwa bidii na maarifa katika sekta za Umma na Binafsi.

    Kauli hiyo imeitoa katika Ziara yake Siku Moja Kisiwani Pemba Wakati kujitambulisha na kuzungumza na Mabaraza ya Wazee wa CCM wa Mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba huko Ukumbi wa Makonyo Wilaya ya Chake Chake.

     Balozi Dkt. Nchimbi, amesema CCM inaendelea kuimarika Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi kutokana na misingi mizuri iliyowekwa na Wazee wa Chama hicho enzi za Utumishi wao toka walipoviunganisha Vyama vya ASP na Tanu na Kuzaliwa kwa CCM Mwaka 1977.

     Aidha Dk. Nchimbi amesema utulivu na umoja uliopo ndani ya CCM ni Matokeo ya kazi kubwa ya kimalezi iliyofanywa na Wazee hao Wakati wa utumishi wao katika Chama hicho

    Naye Naibu Katibu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohamed Said Dimwa Amesema CCM Zanzibar ipo imara na itaendelea kusimamia nakutekeleza Siasa za kistaarabu zinazozingatia ushindani wa kisera kwa vitendo huku ikijiandaa kikamilifu kuhakikisha inapata ushindi katika ngazi zote za Uchaguzi Mkuu ujao.

     Kwa upande wake Katibu wa Mabaraza ya Wazee Mkoa wa Kusini Pemba Bi.Hanuna Ibrahim Massoud amesema wamefurahishwa na Uteuzi wa Katibu Mkuu huyo, kwani ni Kiongozi Mzalendo, mchapakazi na anayekijua Chama cha Mapinduzi kwa ufasaha

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.