Shirika la Reli Tanzania TRC limesema katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Shirika hilo limefanikisha kujenga Kilomita 1,560 za Mradi wa Reli ya kisasa ya SGR.
Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja Kadogosa amesema Thamani ya uwekezaji wa Mradi huo imefikia Trioni 23.3ukiondoa kipande cha Uvinza hadi Musongati ambapo kipo katika hatua ya ununuzi ambapo kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Trioni 10.01 zimeshalipwa kwa Wakandarasi .
Amesema kiujumla utekelezaji wa ujenzi unaoendelea kwa vipande vitano vipya ambapo vitatu ni katika kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza ya Reli SGR kati ya Dar Es Salam hadi Mwanza ambapo ,Makutupora hadi Tabora( km368) Ujenzi umefikia asilimia 13.98,Tabora hadi Isaka( km 165) umefikia asilimia 5.44na Isaka hadi Mwanza( km341) ambapo Ujenzi umefikia asilimia 54.01 .
Akizungumzia Ukarabati wa Reli ya zamani( MGR) Mkurugenzi Kadogosa amesema Serikali ya awamu ya Sita imetowa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Mabehewa zaidi ya Mia Sita kati ya hayo Mabehewa Mia Mbili Tayari yameshafanyiwa ukarabati .
Shirika la Reli Tanzania linaendelea kuhakikisha usafiri wa Abiria na Mizigo unaendelea kwa ufanisi ili kutimiza malengo na maadhimio ya Shirika hilo kwa kutoa huduma bora na yakuaminika ya usafiri wa Reli Nchini.