Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 28 pamoja na Pikipiki 29 ambazo zilikuwa zikitumiwa na watuhumiwa hao kwenye uporaji wa Simu na Vitu vingine kutoka kwa Wananchi Manispaa ya Morogoro.
Kuwepo kwa Waporaji kwa njia ya Pikipiki kuliibua sintofamu kwa Wakazi Manispaa ya Morogoro ambapo kutokana na tatizo hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Sacp Alex Mkama amesema tangu Mwezi Januari hadi Machi Mwaka huu wamefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa wa uporaji pamoja na uporaji.
Kutokana na kukamatwa kwa watuhumiwa hao Kamanda Sacp Mkama amesema malalamiko ya uporaji yamepungua kwa sasa huku baadhi ya Wakazi Manispaa ya Morogoro wakifurashishwa na hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.
stories
standard