Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imetiliana Saini na Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Semuka Mkataba wa Uchapishaji wa Vitabu kwa ajili ya Skuli za Binafsi Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya Utiaji Saini huo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Ali Abdulgulam Hussein amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Wananchi wake wanapata Elimu iliyobora hivyo inachukua juhudi mbalimbali kuimarisha miundombinu ya Elimu.
Wakizungumza mara baada ya Utiaji Saini huo Kiembe Samaki TC Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla Said na Afisa Masoko wa Kampuni Kimataifa ya Semuka Walii Hassan Miyonga wamesema wameona kuna mahitaji makubwa ya Skuli za Binafsi na Serikali hivyo wameamua kutafuta Mchapishaji ambae atafanya kazi ya kuchapa Vitabu hivyo na kutoa kwa Skuli Binafsi na kuahidi kutoa Vitabu hivyo kwa muda usiozidi Miezi Miwili
Naibu Katibu Mtendaji Jumuiya ya Skuli Binafsi ZAPS Ndg.Mbarouk Shaaban Haji kwa niaba ya Walimu Wenziwe wameishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na kwamba wataendelea kushirikiana pamoja ili kukuza Sekta ya Elimu na kuinua Viwango vya Wananfunzi