Waziri wa Fedha na Mipango Drk.Saada Mkuya Salum amewataka Watendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu wa Tigo Zantel kuhakikisha huduma ya Tigo Bima inaendana na Wananchi kwa kuwa na tija na Serikali.
Akizindua huduma mpya ya Tigo Bima kwa Vyombo ya Moto huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza Mapato ya Serikali na kuongeza Uchumi wa Nchi kwa njia ya Kidigitali.
Amesema huduma hiyo imeleta Mapinduzi kwa kuondosha msongamano wa Wananchi kupatiwa huduma za Bima na kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Dk.Saada amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na Sekta Binafsi ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na huduma za Kidigitali.
Mkurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar Arafat Haji amesema huduma hiyo ina lengo la kuleta mageuzi ya huduma za Kidigitali kwa kulipia huduma za Bima kwa Simu za Mkononi kwa njia ya Tigo kwa urahisi
Afisa Mkuu Tigo Pesa Angelica Pesha amesema Mtandao wa Tigo Zantel umechukua hatua ya kuwaletea maendeleo Wananchi kupitia huduma za Kidigitali na kupunguza gharama na mabadiliko ya Teknolojia