HUDUMA YA TIGO BIMA HURAHISISHA MAISHA YA WATANZANIA

Mhe.Saada Mkuya

     Waziri wa Fedha na Mipango Drk.Saada Mkuya Salum amewataka Watendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu wa Tigo Zantel kuhakikisha huduma ya Tigo Bima inaendana na Wananchi  kwa  kuwa na tija na Serikali.

     Akizindua huduma mpya  ya Tigo Bima kwa  Vyombo ya Moto huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege  amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza Mapato ya Serikali na kuongeza  Uchumi wa Nchi kwa njia ya Kidigitali.

     Amesema huduma hiyo imeleta Mapinduzi kwa kuondosha msongamano wa  Wananchi kupatiwa huduma za Bima na kuleta maendeleo kwa Watanzania.

     Dk.Saada amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na Sekta Binafsi  ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na huduma za Kidigitali.   

     Mkurugenzi  wa Shirika la Bima Zanzibar  Arafat Haji amesema huduma hiyo ina lengo la kuleta mageuzi ya  huduma za Kidigitali  kwa kulipia huduma za Bima kwa Simu za Mkononi kwa njia ya Tigo kwa urahisi   

    Afisa Mkuu Tigo Pesa  Angelica Pesha amesema Mtandao wa  Tigo Zantel umechukua hatua ya kuwaletea maendeleo Wananchi kupitia huduma za Kidigitali na kupunguza gharama na mabadiliko ya Teknolojia 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.