SERIKALI KUKABILIANA NA HALI YA UGUMU WA MAISHA KWA WANANCHI

Dk.Mwinyi Wazee

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itachukua jitihada za kukabiliana na hali ya ugumu wa maisha kwa kadri ya hali itakavyoruhusu ili kuwapunguzia mzigo Wananchi.

   Akizungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi katika Ikulu ya Pagali, amesma kupanda kwa gharama za maisha kunachangiwa na matatizo katika uchumi wa Dunia zikiwemo, vita, kupanda bei kwa bidhaa za nje na baadhi ya Mataifa Duniani kuzuia kuuza bidhaa zao kwa Mataifa mengine.

   Hivyo Dk .Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafanya kila linalowezekana kustawisha uchumi na hali za Wananchi.

    Akizungumzia tatizo la Bandari ya Mkoani na hali ya kupanda kwa bei za bidhaa Nchini, Dk.Mwinyi amesema Serikali ina nia ya kuleta Meli ya moja kwa moja kutoka Bandari ya Mombasa hadi Bandari ya Mkoani kwa lengo la kushusha bidhaa ili kupunguza gharama za maisha na mfumko wa bei za bidhaa huku akiwaomba Wazee hao kuendelea kuiombea Nchi ili iendelee kuwa na amani.

    Wazee hao wamempongeza Dk.Mwinyi kwa hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa Nchini ndani ya muda mfupi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.