Wanawake wa Kiislam wametakiwa kuendelea Kuihifadhi Qur-an na kusimamia misingi yake ili kuweza kuleta mabadiliko katika malezi ya Familia zao .
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Mhandisi Zena Ahemed Said ametoa ushauri huo katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Kina Mama Watu Wazima na kuwataka Kusoma Qur-an na kuielewa ili kuacha makatazo yake na misingi bora kwa Jamii kwa kuzingatia Wanawake ndio Walezi wa Familia.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadh Qur-an Kina Mama Watu Wazima Ukhty.Fatma Ibarahim amesema lengo la kuiendeleza Jumuiya hiyo na kushikamana katika kushajihishana kufanya mema
Akisoma Taarifa ya Jumuiya hiyo Ukhty.Asya Haji Juma amesema licha ya kufanikisha kukamilika Mashindano hayo wanakabiliwa na matatizo mbalimbali kama kukosa wasimamizi wa uhakika wa kusimamia Mashindano hayo.