Akizungumza mara baada ya kupokea Taarifa hiyo Rais Samia amesema kuwa ripoti hizo zinazosomwa kila Mwaka zinachangia maboresho katika kuimarisha utendaji kazi kwa Serikali pamoja na Mashirika ya Umma.
Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ndg.Charles Kichere ameishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza miradi mipya ya Barabara.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru CP Salum Rashid Hamduni,amesema Takukuru ilichunguza na kukamilisha majadala 900 yakiwemo 21 ya Rushwa kubwa yaliyohusisha tuhuma za ubadhirifu na hasara kwa Serikali.
stories
standard