Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, imeiomba Serikali kuendelea kuvijengea uwezo Vikosi vya Idara Maalum za SMZ, ili viweze kuimarisha uzalishaji wa Kilimo na ufugaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, Mh Machano Othman Said, akizungumza baada ya kutembelea Vikosi vya Idara Maalum, amesema wamebaini kuwa vikosi hivyo vinaendesha Miradi yake ya uzalishaji bila ya kuwa na Utaalamu wa kutosha na kupelekea kushindwa kujitegemea.
Kuhusiana na Ofisi za Mikoa na Wilaya na Serikali za Mitaa, amewataka Watendaji wake kuwa Wabunifu na Mikakati mizuri, itakayosaidia kumaliza kwa haraka Miradi waliyoanzisha ili iweze kuwasaidia Wananchi na kuleta tija kwa Serikali.
Mh machano, amezitaka Serikali za Mitaa kuandaa Bajeti kwa makini itakayosaidia kutekeleza Miradi ya maendeleo kikamilifu ambayo itaondoa changamoto moja kwa moja kwa Wananchi.
Nae Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na idara maalum za SMZ, Mh masoud Ali Mohammed, amesema Ofisi yake imetoa mafunzo kwa watendaji wake kwa lengo la kujenga uelewa wa sheria na kanuni na miongozo, ili waweze kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.