TAASISI ZA FEDHA NCHINI ZATAKIWA KUWEZESHA MAWAKALA

MH.AYOUB IFTAAR

    Taasisi za Fedha Nchini zimetakiwa kuwawezesha Mawakala kwa kuwapatia Mikopo kwa muda sahihii pale inapohitajika kwa lengo la kuwahudumia Wananchi na kukuza uchumi wa Nchi.

    Akizungumza baada Iftari iliyoandaliwa na Kampuni ya Said Holding huko Mlandege Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh:Ayoub Moh'd Mahmoud amesema hatua hiyo itawezesha Mawakala kukuza uchumi wao  na kulipa Kodi kwa wakati 

    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Said Holding Ndg.Said Issa  Khatib amesema matarajio ya Kampuni hiyo ni kujitanua zaidi kibiashara kwa kukuza na kuimarisha Miamala ya Kifedha

    Muwezeshaji wa Kampuni hiyo Seif Rashid Omar amesema ina lengo lengo la Iftari hiyo ni kuwashajihisha Watu wenye uwezo  kuwasaidia Watu wasiojiweza hasa kwa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.