Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi imesisitiza kusimamiwa vizuri Miradi inayotekelezwa katika Mpango wa kunusuru kaya Masikini Tasaf ili iweze kufikia tija iliyokusudiwa.
Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mwanaasha Khamis Juma wametoa ushauri katika ziara ya kukagua Miradi ya Tasaf iliyotekelezwa Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na kupokea Taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya Masikini kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024.
Wameipongeza Serikali kwa kuendelea kupeleka Fedha katika Miradi yenye Tija kwa Wananchi na kuwasisitiza Watendaji kuhakikisha mpango huo unakwenda sambamba na Mikakati ya Serikali ya kuinua kipato cha Wananchi.
katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dkt. Islam Seif Salum akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Tasaf Zanzibar, amesema mpango huo umeendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa walengwa na kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kubuni Miradi.