Shirika la Reli Tanzania TRC limepokea Kichwa cha kwanza cha Treni chenye Muundo wa mchomoko na uwezo wa kuunganisha Mabehewa nane yenye uwezo wa kubeba abiria Mia Tano na Themanini na Tisa kwa wakati Mmoja.
Akizungumza katika Hafla ya ushushaji Bandarini Jijini Dar-Es-Salaam, Waziri wa uchuzi Mhe Profesa Makame Mbarawa amesema, Kichwa kilichopokelewa ni Miongoni mwa Vichwa Kumi vinavyotengenezwa na Kampuni ya Huindai Rotam ya Nchini Korea ya Kusini.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Amina Lumuli amesema baada ya kukamilika kwa zoezi la ushushaji hatua itakayofuata ni zoezi la majaribio.
Meneja Mradi wa Manunuzi wa Vichwa vya Treni Mchomoko TRC Mhandisi Kelvini Kimario akaelezea Teknolojia iliyotumika katika matengenezo ya Treni kuwa ni mapoja na uwezo wa kumwongoza Dereva kupunguza Mwendo kwenye maeneo yanayotakiwa kupunguzwa Mwendo.