Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al haj Dkt Huseein Mwinyi amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuendeleza mema waliyodumu nayo katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuimarisha ustawi wa Jamii.
Akizungumza katika hafla ya Baraza la Eid huko Ziwani amesema kufanya hivyo kutaweza kuidumisha Nchi katika hali ya Amani na Usalama.
Amefahamisha kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umeacha Somo la Huruma na upendo baina ya Watu hivyo ni vyema kwa Waumini kuyaendeleza ili kuendelea kupata fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Dkt Mwinyi emeliagiza Jeshi la Polisi kuimarisha Ulinzi na usalama katika kipindi cha Siku Kuu ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza
Waziri wa katiba Sheria Utumishi wa umma na Utawala bora Mh Haroun Ali Suleiman amesema ni wajibu wa kila Mwananchi kuwaombea Amani Viongozi wa Kitaifa ili kuendeleza maendeleo
Sheikh Mohammad Othman Mohammed amewataka Waumini kuwa na Subra katika shughuli zao mbalimbali ili kupata Radhi za Mwenyezi Mungu
Siku kuu ya Eid- Elftr husheherekewa kila Mwaka baada ya Waumini wa Dini ya Kiislam kukamilisha Nguzo ya Nne ya Uislam ya kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani