TUME YA KUSHUGHULIKIA HOJA ZA MUUNGANO KUUNDWA

Uzinduzi sherehe za Muungano

       Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nyanja zote za Maendeleo, Kisiasa, Uchumi, Utamaduni na huduma za Jamii yameipatia Nchi heshima kubwa kwenye Jumuiya ya Kimataifa. 

    Dk. Mwinyi ameyasema hayo Viwanja vya Maonesho ya Biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharibi 'b' Wakati wa Uzinduzi wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

     Amesema, kwa Kipindi cha Miaka 60 ya Muungano huo, Tanzania imeendelea kubaki kwenye Historia na Mfano bora wa kudumisha Muungano Barani Afrika na Duniani kote kutokana na Misingi thabiti ya Umoja, Amani na Mshikamano viliyoasisiwa na Viongozi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pamoja na Viongozi wenzao Waasisi wa Muungano huo. 

    Akizungumzia matatizo ya Muungano, Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeendelea kuchukua hatua madhubuti kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya Muungano huo, ikiwemo kuunda Tume na Kamati kwa ajili ya kushughulikia hoja za Muungano.

     Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed  Suleiman Abdulla amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ofisi ya Muungano na mazingira ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zinana wajibu wa kuielewa Jamii juu ya Historia ya Muungano kwa Vizazi viliopo sambamba na kuwasihi Watanzania kuendelea kuu Watanzania.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Dk. Selemani Saidi Jafo amesema Historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeundwa na sababu nyingi hadi kufikia kusainiwa kwa Hati ya Muungano Mwaka 1964 chini ya Waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Julius K. Nyerere na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

    Uzinduzi wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Ufunguzi wa Maonesho Maalum ya Taasisi za Muungano chini ya kaulimbiu, “Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu”, unaashiria kuanza Rasmi kwa shughuli mbalimbali za Kijamii ikiwemo upandaji wa Miti, Usafi wa Mazingira, Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo na Uwekaji wa Mawe ya Msingi kwa Maeneo Mbalimbali ya Tanzania. 

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.