Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaj Hassan Kabeke, amekemea tabia ya baadhi ya Vijana kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya, ikiwemo Mirungi na Mihadarati, zinazotajwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa na kudhoofisha Afya zao
Alhaj Kabeke ametoa onyo hilo katika Hutba ya Eid El Fitri katika Swala ya Eid iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza kufuatia kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mojawapo ya Nguzo kuu ya Dini ya Kiislamu.
Sheikh Kabeke pia amewaomba Watanzania kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika baadaye Mwaka huu.
Baadhi ya waumini walioshiriki Swala ya Eid El Fitri, iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, Wakuu wa Wilaya za Ilemela na Nyamagana wamesema kuporomoka kwa Maadili ndiyo chanzo cha Vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya Dawa za Kulevya.