Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Meh.Leila Mohammed Mussa amewataka Wadau wa Elimu waliohudhuria Mkutano wa 7 wa mabadiliko ya Elimu kwa maendeleo endelevu kuhakikisha urasimu hauchukui nafasi katika uboreshaji wa Sekta ya Elimu Nchini
Ameyasema hayo huko Hoteli ya madinatul Bahri Mbweni, Waziri huyo amewataka Wadau hao kujadili matatizo yaliopo katika Sekta hiyo pamoja na kuyatafutia ufumbuzi.
Aidha amehimiza suala la uwajibikaji kwa Vitendo katika mapendekezo watakayokubaliana kwenye Mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndugu Abdalla Khamis amesema miongoni mwa yatakayojadiliwa katika Mkutano huo ni Tathmini ya Mabadiliko ya Maendeleo ya Elimu ndani ya kipindi cha Mwaka Mmoja.
Khadija Ahmed Sharif, Mdau wa Elimu kutoka Milele Foundation amesema mapendekezo yatakayofikiwa hapo yataleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu.
Mkutano huo wa Siku Mbili ulioanza leo unatarajiwa kujadili mabadiliko mbalimbali ya Elimu hapa Nchini.