WATUMISHI OR TMSMIM KUZINGATIA KANUNI ZA UTUMISHI.

MHE. MASOUD ALI MOHAMMED

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Mhe Masoud Ali Mohammed, amewasisitiza Watumishi wa umma kuwa mfano bora katika kufata misingi na kanuni za Kiutumishi.

 akizungumza na Watendaji wa Ofisi Kuu Ofisini kwake Vuga, ameitaka kila Idara kuhakikisha inajitathmini na kuchukua hatua katika Utendaji wa kazi ili kuweza kufikia malengo bora ya kiutendaji yaliyokusudiwa.

Amesema kufanya kazi kwa ushirikiano ndio Silaha ya kufikia Maamuzi yalio Sahihi, ambayo yatachangia kuleta maendeleo kwa Watendaji hao, Wananchi na Taifa kwa ujumla.

 aidha Waziri Masoud amewataka Watumishi hao kuepuka migogoro katika kazi na badala yake wajiimarishe katika kuongeza Elimu ambayo itasaidia kutimiza wajibu wao katika Utumishi kwa uweledi na ujuzi zaidi.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.