SERIKALI KUTUNGA KANUNI MPYA ZA UTUNZAJI MAZINGIRA

WAZIRI JAFO JAFO

Serikali ipo Mbioni kutunga Kanuni mpya za utunzaji wa Mazingira kwa Wazalishaji wa Vinywaji vinavyotumia Chupa za Plastiki na Vifungashio ambapo Watalazimika kukusanya Chupa zilizotumika kutoka Mitaani kwa lengo la kutunza Mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo,ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Akifungua Kikao cha Majadiliano na Wazalishaji wa Bidhaa zinazofungashwa kwa Plastiki kilichohusu kupata Ufumbuzi wa tatizo Kuzagaa kwa Chupa za Plastiki Mitaani. 

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mazingira,Bi.Christina Mndeme amesema wanaendelea kuratibu na kusimamia Masuala ya uhifadhi wa Mazingira katika kuhakikisha Mazingira yanatunzwa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.