Mvua zinazoendelea kunyesha Maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro kuanzia Mwishoni mwa Mwezi March zimesababisha kuathirika kwa Miundombinu ya Barabara pamoja na Madaraja 9 kutoka Maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro .
Meneja wa Wakala wa Barara za Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro Nicholaus Fransis amesema hayo Wakati Waandishi wa Habari kuhusu athari za Miundombinu ya Madaraja na Barabara zinazotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha , ambapo amesema maeneo yaliyoathirika zaidi katika Mkoa huo ni Wilaya Hai.
Kutokana na Athari hizo tayari Serikali inafuatilia kwa ukaribu na Zaidi ya Bilioni 2.5 zimeshatengwa kwaajili ya kurejesha Miundombinu hiyo iliyoharibika.
Akizungumizia athari katika miundombinu ya Daraja ya Mungushi na Biriri la Mto Sanya amesema tayari Mkandarasi yupo Eneo la kazi kwaajili ya kutoa magogo.