SERIKALI KUIMARISHA USAFIRI WA BARABARANI

DKT KHALID SALUM MOHAMED

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Serikali inaimarisha Sekta ya usafiri wenye uhakika na salama ili kuondosha usumbufu kwa Wananchi.

Akifungungua Mkutano juu ya usalama wa usafiri, Dkt. Khalid amesema uimarishaji huo unaenda pamoja na uimarishaji Miundombinu ya Barabara ili kupunguza Ajali na Msongamano pamoja na kupunguza gharama.

Balozi wa Hispania Nchini Tanzania, Jorge Moragas amesema Serikali ya Nchi hiyo imetoa Euro Milioni 1 Nukta Mbili ili kufanya Stadi ya kuangalia Mfumo mzima wa usafiri na maatizo yanayoikumba sekta hiyo kwa ajili ya kuyatatua.

Mkuu wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi amesema Mradi huo utaweka mikakati imara ili upate ufanisi katika utekelezaji wake.

Mradi wa Idom utatekelezwa kwa kushirikiana na Serikali na Taasisi ya Karume Zanzibar utafanya Stadi ya usafiri ili kulinda mazingira na utachukua Miezi 18.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.