RAIS SAMIA ATUKUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA UDAKTARI

Rais Samia atunukiwa shahada ya heshima

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Nchini Uturuki.

     Rais Dkt.Samia ametunikiwa Shahada hiyo na Mkuu wa Chuo Kikuu Ankara cha Nchini Uturuki na Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo ambapo Rais Samia yupo katika Ziara kazi ya Siku Tano Nchini humo.

     Akizungumza katika Hafala hiyo Rais Samia amesema Tanzania inaitambua mchango wa Uturuki katika G20 Hususani katika masuala ya Afrika ikiwa ni kuweka Kipaumbele kwenye changamoto za Madeni, Marekebisho ya usanifu wa Fedha Duniani na kuhakikisha Fedha za maendeleo endelevu ili kushughulikia ukosefu wa usawa na ukosefu wa haki.

   Kwa upande wao  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara Nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar amesema wameamua kumtunuku Rais Samia Shahada ya Heshima ya Uzamivu" katika fani ya "Uchumi" kutokana na mchango wake Mkubwa katika Maendeleo ya kiuchumi na Mahusiano ya Kibiashara kati ya Jamhuri ya Uturuki na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

   Katika Kipindi cha Miaka 10 iliyopita Nchi hizi Mbili zimeshuhudia ongezeko la Biashara kutoka Dola Milioni 60 Mwaka 2011/2012 hadi dola milioni 300 mwaka 2022/2023.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.