WAZIRI MKUU AMEOMBA USHIRIKIANO KWA WANAOKUSANYA MAONI YA DIRA MPYA YA TAIFA

MHE. KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, amewataka Wakuu wa Mikoa Tanzania Bara na Zanzibar kutoa ushirikiano kwa Timu za Wataalamu wanaokusanya maoni ya Dira mpya ya Taifa katika Mikoa yao ili waweze kupata maoni yenye tija kwa Taifa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo  Jijini Dodoma wakati akifungua Semina ya Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Bara na Zanzibara kuelekea Mchakato wa utoaji Maoni ya Dira ya Taifa ya maendeleo.=

Aidha amewataka kushirikiana na Viongozi wa Dini ili kuweza kufanikisha zoezi hilo la ukusanyaji maoni kwa Wananchi.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo,amesema wameamua kuwashirikisha wakuu wa Mikoa ili kurahisisha zoezi hilo na kuwafikia Wananchi wengi zaidi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.