Habari

SHILINGI BILIONI 1 KUTUMIKA KWA AJILI YA KUSAFISHA MITARO

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Mbili kwa ajili ya kusafisha Mitaro yote ya kupitishia Maji ya Mvua ili kuepusha kuathiri Makaazi ya Watu na Maeneo mengine.

    Akizungumza baada ya kukagua Bwawa la Mwantenga kwa Mtumwa Jeni amesema hatua hiyo itachukuliwa ili kuhakikisha hakuna madhara yanayotokea, hivyo Serikali inatafuta ufumbuzi wa kudumu katika Maeneo ya wazi ili kuondosha kasoro za mafuriko ya Mvua na athari yoyote isitokee kupitia Mradi wa Big-z.

TAASISI YA WASANIFU,WAHANDISI NA WAKADIRIAJI MAJENGO YAZINDULIWA

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inathamini mchango wa Fani za Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji kwenye utekelezaji wa Mipango mikubwa ya Maendeleo hasa Miradi ya Ujenzi.

   Akizindua Taasisi ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Zanzibar huko Hoteli Verde, Mtoni amesema Serikali itaendelea kuwahusisha kikamilifu kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji wa Wataalamu Wazawa katika Miradi endelevu ya kimkakati ya uwekezaji Nchini.

FARAJA YAWAFIKIA WANAFUNZI WA SKULI YA SEKONDARI BWIRO

     Mradi wa kupunguza Umaskini unaotekelezwa na Tasaf, umekamilisha Ujenzi wa Bweni la Wasichana Zaidi ya 100 pamoja na Bwalo la Chakula katika Skuli ya Sekondari Bwiro.

    Mratibu wa Tasaf Wilaya ya Ukerewe Jenitha Byagalama amesema Ujenzi wa Bweni na Bwalo la Chakula kwa pamoja umegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 300 chini ya ufadhili wa Nchi zinazozalisha Mafuta Duniani.

VIFAA VYA KUSHUSHIA MAKONTENA VYAWASILI BANDARI YA MALINDI

    Shirika la Bandari Zanzibar limesema tayari wameshaanza kutatua matatizo yanayolikabili hasa kwenye sehemu ya kushusha mizigo.

    Akizungumza baada ya kupokea Vifaa vipya vya kubebea mizigo huko Malindi Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar Akif Khamis amesema Mashine hizo zitawezesha kutatua matatizo yanayolikabili Shirika hasa kwenye sehemu ya kuchusha mizigo.

     Amesema Vifaa hivyo vina uwezo mkubwa wa kushusha Makontena katika muda mdogo zaidi ukilinganisha na vilivyopo sasa.

MAFANIKIO MAKUBWA YAPATIKANA KATIKA IDARA YA UHAMIAJI NDANI YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kukamilika kwa jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi kutaongeza ari na kasi ya utoaji wa huduma za Uhamiaji katika Mkoa huo na Manispaa zake zote tatu .

     Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja tarehe 19 Aprili 2024 ikiwa ni shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA JIJINI INSTABUL

 

 

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.

 

MSAKO WA MAMBA WAFANYIKA WILAYANI RUFIJI

        Kufuatia changamoto ya wanyama wakali ikiwemo mamba  katika baadhi ya maeneo ya makazi ya watu pamoja na mashamba yaliyokumbwa na mafuriko Wilayani Rufiji Mkoani Pwani,  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA imeanza msako mkali katika mito na mabwawa dhidi ya wanyama hao ili kuwawezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao

RC MAKONDA AKAGUA MAANDALIZI YA MEI MOSI

      Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ametembelea na kukagua maendeleo ya marekebisho ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha, ikiwa ni Maandalizi ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, inayotarajiwa kufanyika Tarehe 01.05. 2024.

     Mgeni wa Heshima katika Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

ZBC YAADHIMISHA KUTIMIA MIAKA 11 YA UTENDAJI TANGU KUANZISHWA KWAKE

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mhe.

TANZANIA BADO HAIKO TAYARI KUTOA URAIA PACHA

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema bado haiko tayari kuwa na utaratibu wa kutoa Uraia Pacha badala yake iko katika hatua za Mwisho kukamilisha utoaji wa Hadhi maalum kwa Raia wa Nchi nyingine wenye Asili ya Tanzania ili kuchangia ipasavyo katika Maendeleo ya Taifa.

    Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati   akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafaniko ya Wizara hiyo katika kipindi cha Miaka 60 ya Muungano Tanganyika na Zanzibar.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.