MSAKO WA MAMBA WAFANYIKA WILAYANI RUFIJI

zoezi la ukamataji wa mamba

        Kufuatia changamoto ya wanyama wakali ikiwemo mamba  katika baadhi ya maeneo ya makazi ya watu pamoja na mashamba yaliyokumbwa na mafuriko Wilayani Rufiji Mkoani Pwani,  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA imeanza msako mkali katika mito na mabwawa dhidi ya wanyama hao ili kuwawezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao

     Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi la uwekaji wa mitego ya kuwanasa Mamba hao huko katika bwawa la ngolobwe  mji mdogo wa utete wilayani Rufiji jana Aprili 18, 2024 afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amesema TAWA inaendelea na msako wa mamba tishio kwa maisha ya watu wilayani humo lengo likiwa ni kulinda  usalama wa wananchi wa wilaya hiyo.

      " Ni wajibu wetu kuimarisha ulinzi ili yasitokee maafa ya binadamu kupotea kutokana na  kuliwa ama kujeruhiwa na mamba wakati  mamlaka ipo kwa ajili yaoKama sheria ya uhifadhi ya wanyamapori sura namba 283 inavyotuelekeza kudhibiti wanyamapori wakali " amesema Maganja.

      Askari wa wanyama pori kutoka Tawa John Mishimo amesema zoezi hilo la usakaji wa mamba katika mto huo wa lugogwe linalofanywa na tawa limetokana na wanyama hao kuhama katika makazi yao kuliko sababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa Nchini ambapo kwa sasa wameonekana kuleta tishio  kwa wananchi.

    Nao baadhi ya wananchi wa mji mji huo mdogo wa utete Wamesema mamba hao wamekuwa changamoto kwa muda mrefu kabla na baada ya mafuriko hivyo jitihada zinazofanywa na tawa katika kuwasaka mamba zimekuwa ni faraja kwao.

 

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.