Habari

STUDIO ZA KISASA ZA KIDIGITALI ZA TBC ZA ZINDULIWA

     WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua studio za kidijiti za redio ikiwa ni sehemu ya mradi wa maboresho ya studio za redio, televisheni na mitandao ya kijamii za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

    Amezindua studio hizo za kisasa (Jumamosi, Aprili 20, 2024) kwenye hafla iliyofanyika kwenye studio za shirika hilo, barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.

DKT.BITEKO AWATAKA WATANZANIA WASIKUBALI KUGAWANYIKA

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewataka Watanzania katu wasikubali kugawanywa kwa namna yoyote na badala yake waulinde na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unatimiza miaka 60 ifikapo tarehe 26 Aprili, 2024 na serehe za maadhimisho yake yatafanyika Jijini Dar es Salaam.

    Dkt. Biteko amesema kuimarika kwa Muungano kumetokana na Amani, utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania na hivyo Muungano ni moja ya Tunu za Taifa ambao unahitaji kulindwa ili kuenzi matunda yaliyopatikana. 

MIAKA 90 YA MZEE MALECELA NI HAZINA YA MAARIFA

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Viongozi na Watanzania wanajifunza mengi kutokana na historia ya utendaji kazi wa Mzee John Samwel Malecela katika nyadhifa mbalimbali alizoshika Serikalini na Chama cha Mapinduzi na ataendelea kuwa hazina muhimu ya maarifa na uzalendo hapa nchini.

DKT.MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA RAIS WA COMORO

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Rais wa visiwa vya Comoro, Azali Assoumani.

    Viongozi hao walikutana leo tarehe 21 Aprili Bweleo, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi .

     Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe 29 Februari, 2024 Dar es Salaam na kuzikwa tarehe 02 Machi 2024 kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

DKT.MPANGO AFUNGUA SKULI YA SEKONDARI MAZIWA NG'OMBE

     Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Philip Isdori Mpango Amesema baada ya miaka 60 ya Muungano, Tanzania inajivunia maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Elimu ambayo inatolewa bila ubaguzi kwa wote.

     Dkt. Mpango ameyasema hayo mara baada ya kufungua Skuli ya Sekondari ya Maziwang’ombe ikiwa ni Muendelezo wa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

AKAUNTI YA NMB PESA ISIYO NA MAKATO YAZINDULIWA KANDA YA KUSINI

    Benki ya NMB kanda ya kusini imezindua kampeni   ya kuhamasisha na kuwawezesha watu wengi kufungua akaunti ili waweze kunufaika na faida za kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa fedha.

    Kampeni hiyo inayoitwa “NMB Pesa Haachwi Mtu” kwa kanda ya kusini imezinduliwa rasmi Mkoani Lindi katika viwanja vya shule ya Msingi Mnolela halmashauri ya Mtama kwa kufanya bonanza la michezo mbalimbali.

    Michezo hiyo ni pamoja na mpira wa miguu,  kukimbia na magunia , kukuna nazi , kunywa soda , mpira wa pete pamoja na mazoezi ya viungo. 

JUMUIYA YA VIJANA NI TEGEMEO KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZI

     Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Jokate Mwegelo, amesema Jumuiya hiyo ni tegemeo katika Chama cha Mapinduzi hivyo atahakikisha inachangia kuleta ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

     Akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi baada ya Mapokezi  yake ikiwa ni Ziara ya kwanza tokea ashike tena wadhifa huo,  Jokate amesema Vijana wana kazi wa kuimarisha Chama hivyo Serikali kwa kuthamini kundi hilo itaendelea kubuni mbinu za kuwawezesha kuzifikia fursa za kiuchumi.

SERIKALI KUANDAA MAFUNZO KWA MAAFISA MANUNUZI

     Maafisa Manunuzi wa Taasisi za Serikali wameishauri Serikali kuandaa Programu za Mafunzo kwa Watendaji ili kufikia lengo la utowaji wa huduma bora.

     Wakizungumza baada ya kumaliza Mafunzo ya Siku 5 juu ya kumtafuta Mshauri elekezi, wamesema kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya huduma kutokana na mabadiliko ya Kidigitali, hivyo kupata mafunzo ni sehemu pekee ya kuimarisha utendaji.

WANAWAKE WAMETAKIWA KUJITOKEZA KATIKA FURSA MBALIMBALI ZINAZOTOKEA NCHINI

    Mke wa Raisi wa Zanzibar   na Mwenyekiti  wa Barazaaza  la  Mapinduzi  Mama Maryam Mwinyi   amewasisitiza Wanawake   kusimama  imara katika Nafasi  zao na kujiamini katika kufanya  Maswala mbali ya kimaendeleo  na kushiriki katika  fursa  zinazotokeya  Nchini.

WAUGUZI WATAKIWA KULETA MABADILIKO SEKTA AFYA

    Wauguzi Wanafunzi wametakiwa kuwajibika na kuhakikisha kuwa wanaleta  mabadiliko katika fani hiyo ili kuongeza hadhi na sifa za Wauguzi hasa kwa walioko kazini.

    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika Mkutano Mkuu wa 18 na Kongamano la Kisayansi lilowashirikisha Wanafunzi Wauguzi kutoka Vyuo Vinane Tanzania Bara na Visiwani, amesema Wauguzi wanaweza kuleta mabadiliko katika huduma za Afya, hivyo ni vyema kuongeza nguvu katika kutoa huduma.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.