WAUGUZI WATAKIWA KULETA MABADILIKO SEKTA AFYA

WAUGUZI

    Wauguzi Wanafunzi wametakiwa kuwajibika na kuhakikisha kuwa wanaleta  mabadiliko katika fani hiyo ili kuongeza hadhi na sifa za Wauguzi hasa kwa walioko kazini.

    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika Mkutano Mkuu wa 18 na Kongamano la Kisayansi lilowashirikisha Wanafunzi Wauguzi kutoka Vyuo Vinane Tanzania Bara na Visiwani, amesema Wauguzi wanaweza kuleta mabadiliko katika huduma za Afya, hivyo ni vyema kuongeza nguvu katika kutoa huduma.

    Mkurugenzi Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Mwanaisha Juma Fakih amesema katika kuimarisha huduma za Afya, ili kuona huduma zinazotolewa zinawanufaisha Wananchi.

   Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Wanafunzi Tanzania, Lunemna Athumani amesema Chama kimeanzishwa kwa dhamira ya kuwakutanisha Wahitimu wote wa Shahada ya Kwanza ya Uuguzi  na Waliopo Masomoni.

    Kwa upande wa Mwanafunzi Godfrey Denis kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Kikuu Shirikishi Muhimbili amesema kutokana na kukua kwa Taaluma ya Uuguzi ni vyema kufanya utafiti ili kukabilina na Maradhi mbali mbali.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.