Habari

MH.HEMED ASHIRIKI KATIKA DUA YA KULIOMBEA TAIFA

     Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki katika Dua ya kuliombea Taifa                           Dua hio iliyoongozwa na Makamu wa   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

11 WAFARIKI NA WENGINE 8 KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTKEA SOMANGA

    Watu 11 wamefariki dunia na wengine 8  kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili kugongana katika eneo la Somanga Wilayani Kilwa mkoani Lindi.

ELIMU YATOLEWA KWA WALIOJIANDIKISHA KUHAMA KWA HIARI HIFADHI YA NGORONGORO

     Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kuwaelimisha wananchi wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari kutumia fidia wanazopata kwa kufanya shughuli za maendeleo ili kuweza kuishi maisha bora na kujitegemea katika maeneo mapya wanayohamia.

DKT.MWINYI ASEMA SMZ ITAAJIRI WALIMU WAPYA PAMOJA NA KUBORESHA MASLAHI YAO

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaajiri walimu wapya wa masomo ya sayansi na itaendelea kuboresha maslahi yao.

      Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Skuli ya ghorofa ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh iliopo Monduli, Wilaya ya Magharibi A , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2024 ikiwa ni shamrashamra za Miaka ya 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

ASMA MWINYI FOUNDATION YAANZA KUTOA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI

   Katika Maadhimosho Ya Miaka 60 Muungano  Taasisi Ya Asma Mwinyi Foundation (AMF) ikiungana na Wizara Ya Elimu, Wizara Ya Maendelea, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamojana Wilaya ya Magharibi B imeanza zoezi lake rasmi leo za kugawa taulo za kike kwa wanafunzi 2000 wa skuli 18 za Wilaya Ya Magharibi B.

    Zoezi hili lina tegemea kugawa taulo za kike kwa wanafunzi zaidi ya 30,000 Tanzania Bara na Zanzibar.

     Asma Mwinyi Foundatio imeanza kugawa taulo za kike kuanzia Wilaya Ya Magharibi B

ZDCEA YATAIFISHA VITU VYENYE THAMANI YA BILLIONI '15'

     Zaidi ya vitu vyenye thamani ya Sh. Billioni 15 vimetaifishwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Zanzibar (ZDCEA) baada ya kubainika kutokana na dawa za kulevya.

      Akizungumza na Waandishi wa habari huko ofisini kwake Migombani wilaya ya Mjini, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Kanal Burhan Zubeir Nassoro amesema watuhumiwa wamebainika kufanya biashara haramu ya dawa za kulevya katika nchi mbalimbali ikiwemo Zanzibar, Tanzania Bara, Afrika, Asia, Ulaya na Marekani.

WAZIRI MKUU AWAAGA VIONGOZI WA DINI SAFARI YA MAJARIBIO YA TRENI - DAR -DODOMA

     WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaaga viongozi wa dini 104 ambao wanaelekea Dodoma kwa treni ya mwendokasi (SGR) kwenda kushiriki ibada maalum ya kuliombea Taifa inayotarajiwa kufanyika kesho, Jumatatu, Aprili 22, 2024.

Treni hiyo imeondoka stesheni ya Dar es Salaam saa 8.53 mchana ikiwa na viongozi hao, waandishi wa habari, waimbaji wa nyimbo za injili na kaswida, viongozi wastaafu wa Serikali, watendaji wa Shirika la Reli nchini, wawakilishi wa ubalozi na watedaji wengine wa Serikali.

BOTI YA DORIA YAZINDULIWA BANDARINI DAR-ES SALAAM

     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza taarifa maalum ya udhibiti wa vitendo vya uvuvi haramu iwasilishwe kabla ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi haijawasilisha hotuba ya Bajeti ya Mwaka 2024/2025.

   Ametoa agizo hilo (Jumapili, Aprili 21, 2024) katika hafla ya uzinduzi wa boti maalum kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika bahari hapa nchini iliyofanyika bandarini jijini Dar es Salaam.

TAKWIMU ZA IDADI YA WATU NI NYEZO MUHIMU KWA MIPANGO YA MAENDELEO

      Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Mh.Ali Suleiman Ameir Mrembo,  amesema Takwimu za idadi ya watu  hapa Nchini ni nyenzo muhimu ya  kupanga, kutekeleza na kufatilia sera na mipango ya maendeleo.

      Akifungua Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, katika Ukumbi wa Chuo cha Polisi Ziwani, amesema Takwimu za Idadi ya Watu zinawezesha kupatikana uwelewa juu ya muundo wa Jamii na Maeneo ya Makaazi, ili kuweza kufanya maamuzi sahihi yanayolenga mahitaji halisi ya Wananchi.

SMZ KUIIMARISHA KADA YA MAABARA

     Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuithamini Kada ya Maabara kuwa ni eneo muhimu la kusaidia uchunguzi wa Maradhi mbalimbali , hivyo imeahidi kuimarisha maslahi ya Wataalamu wa Kada hiyo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.