Habari

MALENGO YA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YAVUKWA KATIKA SEKTA YA BARABARA

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 imeelekeza kujenga kilomita 200 za barabara hadi sasa Serikali imejenga kilomita 800 kwa kuvuka malengo ya ilani hiyo.

      Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Barabara ya maeneo huru ya kiuchumi Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 23 Aprili 2024 ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

DKT.MWINYI AWASILI UWANJA WA NDEGE PEMBA

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Pemba na Kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi na Dini tarehe 23 Aprili 2024.

SERIKALI KUJENGA MIUNDO MBINU WEZESHI YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Ujenzi wa Mindombinu ya Elimu Nchini unalengo la kuimarisha sekta ya Elimu iliyoko kwenye mageuzi makubwa ya maendeleo.

MAKAMU WA RAIS AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KULIOMBEA TAIFA.

Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,amewataka Viongozi wa Dini Nchini kuendelea kuliombea Taifa ili kudumisha tunu ya  Umoja,, Amani na Upendo kwa Watanzania

Ni baadhi ya Viongozi wa Dini walioshiriki katika hafla ya kuliombea Taifa  Jijini Dodoma Makamu wa Rais wa Tanzania  Dkt Philip  Mpango amewaongoza Watanzania na Viongozi wa Serikali akizungumza katika  tukio hilo ,amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana na kuulinda Muungano uliodumu tangu kuasisiwa kwake .

WATU 13 WAMEFARIKI KWA AJALI MKOANI LINDI

Watu 13 Wamefariki Dunia na wengine 6 Wamejeruhiwa vibaya baada ya Basi dogo la Abiria aina ya Hiace kugongana uso kwa uso na Roli la Mafuta kwenye eneo la Somanga Wilaya  kilwa Mkoa wa Lindi.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa Mbili Asubuhi na kuhusisha Basi dogo la Abiria aina ya Hiace lenye namba za usajili t 707 DSX lililokuwa likitokea Somanga kuelekea Kilwa Kivinje na Roli la Mafuta lenye Namba za usajili t 224 dzt lenye Tela namba t 920 CUK lililokuwa likitokea Mtwara kuelekea Dar Es Salaam.

BARAZA LA SANAA SENSA YA FILAMU NA UTAMADUNI KUSIMAMIA UTAMADUNI

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita amewataka Wajumbe wa bodi ya Baraza la sanaa Sensa ya Filamu na utamaduni kua na mikakati ya kusimamia Utamaduni Mila na Silka za Kizanzibari katika kutimiza majukumu yao.

Akizindua Bodi mpya ya Baraza la sana Sensa ya Filamu na Utamaduni katika Kikao cha Kwanza cha Bodi hiyo Waziri Tabia amesema ni vyema kutatua matatizo ya wasani ambayo wanaweza kuyatekeleza kwa ufanisi ili kuendeleza na kulinda maadili ya Kizanzibariii  

WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI KUHAKIKISHA WIZARA INAONDOKANA NA UJENZI HOLELA

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Rahma Kassim Ali amesema kuwa kukamilika kwa Kanuni za uhaulishaji Ardhi kutasaidia kuepuka ujenzi holela Nchini 

Akizungumza katika Kikao cha kamati Tendaji kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo kinachojadili mikakati mbali mbali ikiwemo uhaulishaji wa Ardhi na kupitia sheria za Vibali vya ujenzi.

DKT. KHALID ATEMBELEA BARABARA ZILIZOATHIRIKA KWA MVUA

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema kuwa Barabara ya Tunguu,  Makunduchi inatarajiwa kujenga  hivi Karibuni. 

Dkt. Khalid amesema hayo katika ziara ya kutembelea Barabara zilizoatharika  kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha hapa Nchini.

Katika ziara hiyo pamoja na Viongezi wengine wa Wizara yake walitembelea Barabara ya Tunguu -Makunduchi, Kitogani, paje na Bwejuu katika Mkoa wa Kusini Unguja na kuona Barabara hizo zilivyoathirika. 

WANAOKIMBILIA MAENEO YA AJALI KWA LENGO LA KUIBA WAPEWA ONYO KALI

     Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na tabia ya kukimbilia katika maeneo zinapotokea ajali huku wakiwa na lengo la kuwaibia waathirika wa ajali hizo na wakati mwingine kufanya uharibifu.

     Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi,Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema jamii inapaswa kuachana na tabia na vitendo hivyo ambavyo ni hatarishi kwa maisha na mali ambazo zimekuwa zikihusika katika ajali hizo.

DKT.MWINYI AWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KWA MAENDELEO YA NCHI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kushikamana, kuwa wamoja, kudumisha amani na utulivu ili kuzidi kupiga hatua ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini.

      Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea Mwanachuoni mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa Malindi , Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2024.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.