Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Rahma Kassim Ali amesema kuwa kukamilika kwa Kanuni za uhaulishaji Ardhi kutasaidia kuepuka ujenzi holela Nchini
Akizungumza katika Kikao cha kamati Tendaji kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo kinachojadili mikakati mbali mbali ikiwemo uhaulishaji wa Ardhi na kupitia sheria za Vibali vya ujenzi.
Mhe.Rahma amefahamisha kuwa maeneo mengi hayako vizuri kutokana na kukithiri kwa ujenzi holela hivyo ni vyema Watendaji kuhakikisha maazimio yaliyofikiwa yanafanyiwa kazi ili malengo ya utendaji yafikiwe.
Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji Muchi Juma Ameir amesema kuanzishwa Mamlaka ya usimamizi wa vibali vya ujenzi kutasaidia kufanyakazi kwa ufanisi.
Katika Kikao hicho kilijadili kanuni ya uhaulishaji,mabadiliko ya Logo ya Shirika la Nyumba Zanzibar,pamoja na kujadili muongozo wa kamati.