WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI KUHAKIKISHA WIZARA INAONDOKANA NA UJENZI HOLELA

WAZIRI RAHMA KASSIM

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Rahma Kassim Ali amesema kuwa kukamilika kwa Kanuni za uhaulishaji Ardhi kutasaidia kuepuka ujenzi holela Nchini 

Akizungumza katika Kikao cha kamati Tendaji kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo kinachojadili mikakati mbali mbali ikiwemo uhaulishaji wa Ardhi na kupitia sheria za Vibali vya ujenzi.

Mhe.Rahma amefahamisha kuwa maeneo mengi hayako vizuri kutokana na  kukithiri kwa ujenzi holela hivyo ni vyema Watendaji kuhakikisha maazimio yaliyofikiwa yanafanyiwa kazi ili malengo ya utendaji yafikiwe. 

Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji Muchi Juma Ameir amesema kuanzishwa Mamlaka ya usimamizi wa vibali vya ujenzi kutasaidia  kufanyakazi kwa ufanisi. 

Katika Kikao hicho kilijadili kanuni ya uhaulishaji,mabadiliko ya Logo ya Shirika la Nyumba Zanzibar,pamoja na kujadili muongozo wa kamati.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.