Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,amewataka Viongozi wa Dini Nchini kuendelea kuliombea Taifa ili kudumisha tunu ya Umoja,, Amani na Upendo kwa Watanzania
Ni baadhi ya Viongozi wa Dini walioshiriki katika hafla ya kuliombea Taifa Jijini Dodoma Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango amewaongoza Watanzania na Viongozi wa Serikali akizungumza katika tukio hilo ,amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana na kuulinda Muungano uliodumu tangu kuasisiwa kwake .
Aidha Dkt.Mpango amewataka Watanzania kuendelea kulinda na kutunza Mazingira pamoja.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,amewataka Watanzania kuendelea kuulinda na kuutetea Muungano wa Tanzania .
Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Mhe.Dkt. Selemani Jafo,amewapongeza Viongozi wa Serikali zote Mbili kwa kuendelea kutatua hoja za Muungano.