Habari

JAMII YA WAFUGAJI WA CHALINZE WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KWA KUWA WALINZI ILI KUZUIA WIZI WA MIFUGO

     Jamii ya wafugaji wilayani Chalinze wametakiwa kuwajibika kwa kuwa walinzi wa kwanza wa mifugo yao ili kuzuia wimbi la wizi wa mifugo.

      Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa mifugo (STPU) Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Polisi Ally Masimike alipokua akitoa elimu ya kuzuia wizi wa mifugo kwa wafugaji na wafanyabiashara wa nyama katika mnada wa Chamakweza, Wilayani Chalinze, Aprili 24,2024.

DKT.MWINYI AHIMIZA WATOTO KUFUNDISHWA HISTORIA YA MUUNGANO

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuna wajibu wa kuwaenzi waasisi wetu kwa kuweka Kumbukumbu zao, pia amehimiza kufundisha watoto historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

BASHUNGWA AOMBA KULETEWA MAJINA YA MAMENEJA WAZEMBE TEMESA

     Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala kuwasilisha majina ya Mameneja wa Kanda na Mikoa wa TEMESA ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi ili waweze kuchukuliwa hatua.

WAZIRI MKUU AWAONYA VIKALI VIONGOZI WANAOGAWA MAENEO YA STENDI YA KANGE

     WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameonya viongozi wanaogawa maeneo kwenye kitega uchumi kipya cha Dkt. Samia Suluhu Hassan Business Centre kilichopo stendi ya Kange, nje kidogo ya Jiji la Tanga wajiepushe na vitendo vya rushwa.

DKT.NCHIMBI AWAOMBA WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

     Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Katika mambo yote mazuri ambayo anayafanya hasa katika kuleta maendeleo katika Taifa Lenye Amani Upendo na Utulivu pia

     Dkt. Nchimbi amesema Chama Cha Mapinduzi CCM kitahakikisha kinamshauri vyema Mwenyekiti wa chama hicho ili kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGONGORO YASEMA HAKUNA MWANANCHI ATAKAYEPATA NYUMBA KINYUME NA UTARATIBU

     Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kwamba ipo makini kuhakikisha kuwa kila kaya inayojiandikisha kuhama kwa hiyari ndani ya hifadhi inapata nyumba katika Kijiji cha Msomera  kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na kwamba hakuna mtu atakayeweza kupata nyumba kwa njia za udanganyifu.

ZOEZI LA UGAWAJI WA TAULO ZA KIKE LAENDELEA KWA WILAYA YA KATI NA MAGHARIB 'A'

     Asma Mwinyi Foundation (AMF) imeendelea kuunga mkono Serikali zote mbili katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano leo 23.04.2024 imeendelea kuwastiri wanafunzi 2000 kwa kuwapatia  taulo za kike kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali wa Wilaya ya Magharibi A na Wilaya ya Kati kwa kila Mwanafunzi kupatiwa paketi 6 zitakazo wakidhi kwa miezi 6.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO

       Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kigezo cha ziada ya kuzipima Halmashauri zote nchini kuanzia mwaka wa fedha ujao ni kila Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato kuanzia viwili na kuendelea kwa kila mwaka wa fedha.

     Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kufungua Mkutano wa 38 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa - ALAT Taifa unaofanyika Zanzibar.

MADAKTARI BINGWA KUWEKA KAMBI SONGEA (HOMSO)

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, Dkt Magafu Majura amesema kuwa wanatarajia kupokea jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali za Rufaa za mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe.

    Akizungumza mapema hii leo 23/04/2024 ofisini kwake amesema kuwa wanatarajia kupokea madaktari bingwa ambao watatoa huduma za kibingwa na  ubobezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO).

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA AFYA 'CBM'

     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Aprili 23, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali, linalojihusisha na Afya ya Macho Jumuishi na Watu Wenye Ulemavu, 'Christian Blind Mission' (CBM).

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.