Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, Dkt Magafu Majura amesema kuwa wanatarajia kupokea jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali za Rufaa za mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe.
Akizungumza mapema hii leo 23/04/2024 ofisini kwake amesema kuwa wanatarajia kupokea madaktari bingwa ambao watatoa huduma za kibingwa na ubobezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO).
Dkt Majura amesema katika kambi hiyo kutatolewa huduma mbalimbali za kibingwa za akina mama na uzazi, huduma za magonjwa ya watoto, hudumaza kibingwa za magonjwa ya ndani kama vile kisukari, shindikizo la damu, figo na moyo, huduma za upasuaji na mifupa, huduma za macho, huduma za Afya ya akili, huduma za kinywa na meno, huduma za masikio, pua na koo, huduma za ngozi, huduma za mfumo wa chakula, huduma za moyo kwa watoto, huduma za saratani.