Habari

SMZ NA SAUDIARABIA KUENDELEZA USHIRIKIANO

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi  ameihakikishia Serikali ya Saudi Arabia ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi ya maendeleo.

    Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania, Yahya Ahmad Okeish na Ujumbe wake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Nchi mbili hizo.

WATOTO WASISITIZWA KUWA MAKINI NA ATHARI ZA MVUA

     Watoto wa kijiji cha Uwandani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kuzingatia usalama wao kwanza katika kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha hasa wanapokwenda mtoni kwa ajili ya kuogelea na kucheza ili kujiepusha na madhara yanayosababishwa na mvua hizo.

RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.

DKT.MWINYI ASEMA ZANZIBAR ITAENDELEA KUDUMISHA MUUNGANO

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kuwa muumini wa dhati wa Muungano kwa kuudumisha na kuuimarisha kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.

     Rais Dk.Mwinyi akizungumza katika kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yalioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 , Aprili 2024.

WALIOJICHUKULIA SHERIA MIKONONI KWA WAKAAZI WA ENGIKARET WILAYA YA LONGIDO KUSAKWA

     Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo kimesema hakuna sheria inayomruhusu mtu yoyote kujichukulia sheria Mkononi huku likibainisha kuwa tayari linayomajina ya watu waliojichukulia sheria Mkononi na kubomoa nyumba na kuchukua mifugo ya wakazi wa Engikaret Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha.

RAIS DKT. MWINYI AKIRI KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUFANIKISHA KUFANYIKA KWA MUUNGANO

       Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Wanawake walikuwa na mchango mkubwa kufanikisha kufanyika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuzingatia tulipotoka, tulipo na tunakolekea katika harakati za historia ya nchi yetu .

MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO INA LENGO LA KUBORESHA MAISHA YA KILA MWANANCHI WA TARAFA HIYO

       Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kuwa ina lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tarafa hiyo kwa kuwaelimisha na kuwahamisha wananchi waliojiandikisha kuhama kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga na maeneo mengine nchini.

UAMINIFU NA UADILIFU KATIKA KAZI ZA UCHUNGUZI (MAABARA) HUMTOA MWANANCHI WASIWASI KWA KUPATA MAJIBU SAHIHI

      Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amewataka Mawakala wa Maabara ya Serikali kuendelea kuwa waaminifu na waadilifu katika kazi zao za kiuchunguzi wa matatizo ili wananchi waamini majibu yanayotolewa na taasisi hiyo.

       Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Shekh Idriss Abdul-wakil Kikwajuni katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Vinasaba Duniani.

WANAWAKE 6,500 HUFARIKI KILA MWAKA KUTOKANA NA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

     WANAWAKE Zaidi ya 9,500 kati ya 100,000 hugundulika kila mwaka kuwa na tatizo la saratani ya mlango wa kizazi,kati yao wanawake 6,500 hufariki dunia kila mwaka.

      Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko wakati anatoa taarifa ya maadhimisho ya wiki ya chanjo na uzinduzi wa dozi moja ya chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

BILLION 66 KUTUMIKA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZILIZOHARIBIKA

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.

       Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.