Habari

TMA YAPONGEZWA KWA KUIMARISHA UBORA NA USAHIHI WA UTOAJI TAARIFA

      Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wamekutana kupitia kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa TMA kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF, Morogoro Tarehe 30 Aprili 2024, kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi wa Mamlaka kwa kuzingatia maazimio ya Baraza lililopita pamoja na kupitia bajeti ya mwaka 2024/2025. Baraza hilo lilifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari.

DKT.MPANGO AWASILI MKOANI ARUSHA

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewasili Arusha tayari kwa kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani yanayotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha.

DKT.MWINYI AWASILI PEMBA KWA ZIARA YA KIKAZI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Pemba kwa ziara ya kikazi

     Dk. Mwinyi amepokelewa na Wakuu wa Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba, Mhe. Mattar Zahor Masoud na Salama  Mbarouk Khatibu, viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, leo tarehe 30 Aprili 2024.

SERIKALI IMEFANIKIWA KUIMARISHA MIFUMO, SERA NA SHERIA ZA UWEKEZAJI.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua asemina maalum ya uwekezaji kwenye Kilimo iliyoandaliwa na benki ya CRDB Jijini Dar Es Salaam.

Amesema Serikali imeimarisha utoaji huduma kwa wawekezaji kwa kuimarisha Kituo cha utoaji wa huduma za mahali pamoja kilichoko TIC ambapo kwa sasa Taasisi 14 za Serikali zinatoa huduma katika Kituo cha mahali pamoja. 

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Sekta ya Uvuvi imeendelea kuimarika kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali.

KAMPUNI YA CCECC IMETAKIWA KUKAMILISHA MASUALA YA UJENZI WA BARABARA

Wakala wa Barabara Zanzibar Zanroad imetoa maagizo kadhaa kwa Mkandarasi anaejengea Barabara zenye urefu wa Kilomita 100.9 katika Mkoa wa Mjini Magharibi Kampuni ya CCECC ya China, kuchukuwa hatua za dharura kuweka alama za usalama katika mpindo wa Kiembesamaki kwa butros kutokana na Eneo hilo kuwa na Msongamano wa Gari.

POLISI TANZANIA KUSHIRIKIANA NA POLISI WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi za Falme za Kiarabu kutatoa fursa za kubadilishana uzoefu baina ya pande mbili hizo na  kuimarika kwa ulinzi katika Miradi ya maendeleo Nchini. 

Akizungumza na Balozi mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu  Mhe. Saleh Ahmed Alhemeiri, CP Hamad ameomba uwezekano wa kuongezewa taaluma kwa Askari wa Jeshi la Polisi  kuhusiana na makosa ya Kimtandao makossa ambayo yamekuwa changamoto Duniani.

WASICHANA WA KIKE KUPEWA MAFUNZO YA TEHAMA.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dr Khalid Salum Mohamed amesema mageuzi ya Kidigitali yanakwenda kwa kasi   hivyo ni vyema matumizi ya Teknologia  yakatumika ipasavyo.

Akifunga Mafunzo ya Wiki moja  na Mashindano ya Tehama kwa Wasichana huko golden tulip Uwanja wa Ndege Dr Khalid amesema  ni muhimu kuwepo na matokeo ya Teknologia hiyo kwani bado Teknologiajia ya utoaji wa huduma haijatumika ipasavyo. 

MAMA LISHE PEMBA WAKABIDHIWA MITUNGI YA GESI

Afisa Mdhamin Wizara ya kazi uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Dk.Fadhila Abdallah Hassan amewataka Wanawake kubuni mbinu mbalimbali ambazo zitawasaidia katika kupiga hatua mbele za kimaendeleo ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia ya kujiinua kiuchumi.

Dr Fadhila amesema hayo huko Pujini wakati wa ugawaji wa vitendea kazi kwa

Wanawake wanao jishughulisha na Shughuli mbali mbali za Mama Lishe Kisiwani Pemba Vilivyotolewa kwa ushirikiano wa Cocacola ,Orxy gesi, Zbc pamoja na wakala wa uwezeshaji kiuchumi Zanzibar.

CHINA KUSHIRIKIANA NA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Zanzibar, imetiliana Saini ya makubaliano ya Ushirikiano na Chuo cha Taifa cha Afya cha Beijing China.

Kupitia makubaliano hayo yaliyotiwa Saini na Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Chuo Kikuu cha Zanzibar Suza, Dkt. Salma Abdi Mahmoud na Kiongozi wa Timu ya 33 ya Madaktari kutoka China Prof. Jiang Guoging, Wanafunzi na wanataaluma wa Skuli hiyo watapata fursa ya kujengewa uwezo pamoja na fursa nyengine.

TIC IMEKUWA INJINI YA KUTEKELEZA MAONO YA DKT.SAMIA

      WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi na wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kuwa injini ya kutekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muuumgano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga Tanzania yenye mvuto kwa wawekezaji wote.

       “Hatua ambayo nchi yetu imefikia kwa sasa, inaondoa shaka kwa wawekezaji na imeendelea kuthibitisha kuwa nchi yetu ni salama kwa wote waliotayari kuwekeza mitaji yao. Endeleeni kuwa wabunifu, kuimarisha utoaji huduma na kukidhi mahitaji ya ushindani katika masoko ya uwekezaji.”

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.