CHINA KUSHIRIKIANA NA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

SAINI CHINA-CHUO AFYA

Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Zanzibar, imetiliana Saini ya makubaliano ya Ushirikiano na Chuo cha Taifa cha Afya cha Beijing China.

Kupitia makubaliano hayo yaliyotiwa Saini na Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Chuo Kikuu cha Zanzibar Suza, Dkt. Salma Abdi Mahmoud na Kiongozi wa Timu ya 33 ya Madaktari kutoka China Prof. Jiang Guoging, Wanafunzi na wanataaluma wa Skuli hiyo watapata fursa ya kujengewa uwezo pamoja na fursa nyengine.

Jiang Guoging, amesema kupitia Taaluma na uzoefu walionao watahakikisha Wanafunzi wananufaika kupitia makubaliano hayo.

Tukio hilo ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Zanzibar ambao umefikisha Miaka 60.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.