SERIKALI IMEFANIKIWA KUIMARISHA MIFUMO, SERA NA SHERIA ZA UWEKEZAJI.

MHE. KASSIM MAJALIWA

Waziri Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua asemina maalum ya uwekezaji kwenye Kilimo iliyoandaliwa na benki ya CRDB Jijini Dar Es Salaam.

Amesema Serikali imeimarisha utoaji huduma kwa wawekezaji kwa kuimarisha Kituo cha utoaji wa huduma za mahali pamoja kilichoko TIC ambapo kwa sasa Taasisi 14 za Serikali zinatoa huduma katika Kituo cha mahali pamoja. 

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Sekta ya Uvuvi imeendelea kuimarika kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali.

Nae Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ali Othman amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imenufaika na uwezeshaji unaoganywa na Benki ya CRDB Kwa kuwanufaisha Wavuvi na Wakulima wa zao la Mwani

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema Benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza wawekezaji kwa Kuendelea kuwawezesha mitaji pamoja na kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji Nchini

Semina hiyo imewakutanisha Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi pamoja nawazalishaji wa zana za kilimo na Mifugo

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.