Wakala wa Barabara Zanzibar Zanroad imetoa maagizo kadhaa kwa Mkandarasi anaejengea Barabara zenye urefu wa Kilomita 100.9 katika Mkoa wa Mjini Magharibi Kampuni ya CCECC ya China, kuchukuwa hatua za dharura kuweka alama za usalama katika mpindo wa Kiembesamaki kwa butros kutokana na Eneo hilo kuwa na Msongamano wa Gari.
Katika Ziara iliyofanywa na Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Barabara Zanzibar Mhandisi Cosmas Masolwa, ambayo imehusisha Barabara kadhaa zikiwemo Uwanja wa Ndege, Chukwani na maeneo mengine, amesema kutokana na eneo hilo kuwa lango Kuu la kuingia Zanzibar, ameitaka Kampuni hiyo ichukue hatua za haraka ili kulinda Usalama wa Watu.
Aidha ametaka kusafishwa eneo linalotuama Maji katika Barabara ya Uwanja wa Ndege pamoja na kufikiria njia ya kuzuia Maji hayo yasituame pamoja na kuhakikisha Barabara zote zilizokuwa hazitatiwa Lami kuwekewa Kifusi ili kuondosha usumbufu hasa baada ya kuchimbika kwa Mvua.
Wakitolea ufafanuzi Maagizo ya Mkurugenzi huyo Mshauri elekezi wa Mradi wa Barabara hizo Rabih Osseiran amesema atahkikisha maagizo hayo yanatekelezwa kwa wakati huku Kampuni ya CCECC ikiahidi kuchukuwa hatua kwa haraka kwa matatizo yote yanayohusu Mrasi huo.